Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar


Kadri siku zinavyokwenda katika Jamii kunaongezeko kubwa la wanawake kujikita katika nafasi za uongozi pasipo na dosari yeyote.
Kwani kuwepo kwa Uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia imezidi kuleta hamasa kubwa kwa wanawake nchini kuzidi kujipa uaminifu katika kuwania kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Nimefanikiwa kupata bahati ya kuzungumza na baadhi ya wanawake waliobahatika kushika nafasi za uongozi.
Akizungumza na habari za mitandaoni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Jimbo la Fuoni Wilaya ya Magharib B Unguja Amina Hassan Ameir amesema baada ya kupata nafasi iyo ya uongongozi kuna mafanikio makubwa wameyapata ikiwemo kutatua migogoro mbalimbali katika jamii ikiwemo udhalilichaji.''hivi juzi tu kuna mwanafunzi wa form six skuli ya Fuoni amedhalilishwa kwa kupigwa vibaya na mwalimuwake kitendo hicho hatukukifumbia macho tukapambana nacho hadi kufika hatua nzuri ya maamuzi''amesema Bi Amina.
Hatahivyo amesema wamefanikiwa kutembelea sehemu mbali mbali kitendo ambacho kimeweza kuwafumbua macho kwa kuyajua mambo mbali mbali katika jamii.
Pia amebainisha katika uongozi wake wameweza kuwasaidia wazee pamoja na watoto walio na mahitaji maalumu '' Siku maalumu tunajipanga kwa kwenda kula chakula cha mchana pamoja naowatoto hao'' amesema Bi Biamina.
Bi Amina ambae ni mwenyekiti wa UWT tangu ashike nafasi hiyo ya uongozi sasa ni takriban mwaka mmoja na tangu kuongoza kwake imefanikiwa kutatua chagamoto mbali mbli kwa kuzifikisaha sehemu husika na kupata kutatuliwa changamoto hizo.
Nae katibu wa UWT wa Jimbo hilo ndugu Rehema Ali Ubwa amesema katiki jimbo hilo imefanikiwa kupata wanachama wasiopungua elfu tano ambao waliojiunga katika jumuia hiyo.

Amesema malengo waliyonayo kwasasa ni kukaa pamoja na wanachama wake na kujadili jambo gani lakufanya ambalo litaleta tija na kupatikana maendeleo yakudumu.
''Nimekaa kitako na wanachama wangu tukaamua kuwa tufanye wazo la kukopa na kurejesha biashara ndogo ndogo ili baadae inaweza ikakua nakuulikana kwa viongozi wa juu na kutusaidia miundombinu mengine'' amesema
Kwaupande mwengine amewashauri kinamama kujitokeza kwa wingi kuchukua kadi za uanachama ili iweze kuleta maendeleo na mafanikio nchini.
'' Minataka wanawake wajitokeze kwa wingi waangalie mfano wa Rais wetu wa Tanzania alivyokua akipambana na uongozi''
Ndugu Rehema ingawa yeye ni katibu wa Jumuiya ya umoja umoja wa wanawake Tanzania UWT pia amefanikiwa kupata nafasi ya kuwa naibu sheha napia nafasi ya mwenezi wa wadi napia aligombea nafasi ya udiwani wa vitimaalumu
''Niligombea nafasi ya viti maalumu nikapata kura 33 nashukuru kwa kupata kuta hizo maana sijatarajia na kunawezangu hawakupata hata izo wamepata tano nazaidi yapo''
Akizungumza kuhisu malengo yake ya baadae amesema analengo la kugimbania nafasi mbalimbali zajuu ili kutimiza ndoto zake za baadae.''misitokomaa hapa hapa tu lebgo langu ni kupambana kugombea nafasi mbali mbali na kuhakikisha lengo langu linatimia''amesema
Kwaupande wao baadhi ya wanachama katika Jumuiya hiyo wamebainisha kuwa katika jumuiya hiyo kunafaida kubwa wanayoipata kwani inajenga udugu naumoja pamoja na kujua mtatizo mbali mbali yaliyopo kwenye jamii kwaiyo ipo haja ya wanawake kujitowa kwa kujitikeza kwawingi kujiunga ili kupata maendeleo.
See Insights
Boost a Post
Like
Comment
Share