Imeandikwa na Fatma Abrahman - Pembaa`

Wazara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema maandalizi kwa ajili ya mitihani ya taifa ya Zanzibar kwa darasa la Nne, la Saba na Kidato cha pili yamekamilika ambapo jumla ya wanafunzi elfu orobaini na nne, mia sita na themanini na nne wa darasa la 7 wanatarajiwa kuanza mitihani yao kuanzia Jumatatu ya tarehe 30 Oktoba ambapo jumla ya vituo 451 vimesajiliwa kutumika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari huko katika Ofisi za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Waziri wa Wizara hiyo Leila Mohammed Mussa amesema kuwa kwa upande wa wanafunzi wa darasa la 4 jumla ya watahiniwa ni elfu 58, mia 4 na themanini na tano na watafanya mitihani yao kuanzia tarehe 6 mpaka tarehe 8 Novemba na jumla ya vituo vilivyosajiliwa kwa ajili yao wat ni 545.
Kwa upande wa kidato cha pili amesema mitihani imepangwa kuanza tarehe 4 hadi 12 Disemba ambapo jumla ya watihaniwa ishirini na nne elfu, mia tatu na themanini na mbili wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo na vituo vilivyosajiliwa kwa mwaka huu ni 313 kwa Unguja na Pemba.
Aidha Waziri Leala amesema kuwa kwa watahaniwa wenye mahitaji maalum wameandaliwa mazingira ya kufanya mitihani yao kwa mujibu mahitaji waliyonayo ambapo kwa wenye uoni hafifu wameandaliwa mitihani kwa hati zilizokuzwa, huku wenye ulemavu wa uoni watafanya mitihani maalumu kwa kutumia maandishi ya nukta nundu.
Amesema kuwa kwa mwaka huu jumla ya watahaniwa 655 wenye mahitaji maalum wamesajiliwa kufanya mitihani ambapo kwa upande wa darasa la nne ni 289, darasa la saba ni 242 na kidato cha pili ni 124.
Hata hivyo Waziri Leila ametoa wito kwa walimu wakuu wa vituo na wasimamizi wa mitihani kufanya kazi kwa umakini na uadilifu kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya baraza la mitihani na kutoa onyo kwa wakuu wa vituo na waalimu wakuu hasa wa skuli binafsi watakaoingilia kwa namna yoyote vituo vya mitihani na kupelekea udanganyifu.
See Insights
Boost a Post
Like
Comment
Share