Imeandikwa na Fatma Abrahman- Pembaa`
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii tawi la Pemba Nd Saidi Salum Maalim amewataka wanajamii kushiriki katika harakati mbali mbali za usafi wa mazingira katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea visiwani Zanzibar
Ameyasema hayo mara baada ya kufanyika zoezi la usafi lililofanywa na vijana kutoka katika kampuni ya bin issa ilipo tibirinzi chake chake Pemba na kusema kuwa kampuni hio imeonesha moyo wa kizalendo pamoja na kuwaahidi kuwaunga mkono ili kufikia malengo ya kampuni hio .
Aidha amewapongeza vijana kwa kujitolea kwao na kuzitaka kampuni nyengine kuiga mfano kutoka kwao ili kuhakikisha mazingira ya miji na vijijini inakuwa katika hali ya usafi .
Kwa upande wake Afisa Ugavi na Manunuzi Ahmed Omar Iddi amesema lengo la kufanya usafi katika shirika la mfuko wa hifadhi wa jamii ni kuishajihisha jamii kufanya usafi katika kipindi hichi cha mvua zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wa kampuni ya bin issa Ilham Mabrouk Khamis amesema kuwa wameamua kujitolea kufanya usafi katika shirika hilo ikiwa ni katika kufuata maagizo ya Mh Rais Wa Zanzibar ya kutaka Kuiweka miji katika usafi .
0 Comments