Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar
Kila ifikapo tarehe 18 Novembe kila mwaka Ofisi ya mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar inaungana na nchi nyengine barani Afrika kwa kuadhimisha siku ya TAKWIMU AFRIKA.
Hayo yameelezwa leo tarehe 13 Novemba 2023na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salum Kassim Ali akizunhumza na waabdishi wa habari kuko Ofisi ya Mtakwimu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mazizini Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema Tanzania kwaujumla ni miongoni mwa nchi za Afrika ambayo inaadhimisha siku hiyo kupitia Ofisi zake za Takwimu ambapo Siku ya Takwimu Afrika nitukio la kila mwaka ili kuongeza ufahamu wa umma kuhusu umuhimu wa takwimu katika nyanja zote za maisha ya kijamii na uchumi.
Hata hivyo amesema kuelekea katika maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali imeandaa wiki ya maadhimisho ambayo itakua na matukio mbali mbali yatakayowashirikisha watakwimu na wadau mbali mbali kwa lengo la kuongeza uelewa kwa jamii juu ya umuhimu wa Takwimu na maelezo yake.
Amèeleza kuwa madhumuni ya wiki ya maadhimisho hayo ni kutoa muamko kwa wadau na jamii kwa ujumla na kutambua masuala ya takwimu na kuzidisha mashirikiano kati ya watakwimu na wadau wa Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali pamoja na wanajamii kwaujumla ambao ndio wadau wakubwa katika kazi za ukusanyaji wa wa taarifa za kitakwimu zinazotumika katika mipango ya kimaendeleo.
Ameendelea kwa kusema kuwa ndani ya wiki hiyo kutakua na matukio mbali mbali kwa lengo la kueka hamasa na kuzidisha utekelezaji wa majukumu ambayo hutumika kama kigezo cha kupima mafanikio na changamoto mbali mbali zautekelezaji.

Akiyataja matukio hayo katika wiki hiyo amesema kuwa tukio la kwanza ni kuzungumza na waandishi wa habari,kueka kikao cha wastaafu wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Unguja,kuwatembelea wagonjwa waliokuwa watumishi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali,mjadala wa wadau kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho,kikao cha wastaafu Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Pemba pamoja na kuwatembelea Wazèe Sebleni na Welezo.
Amesema siku ya tarehe 18/11/2023 ni siku ya kilele cha maadhimisho ya Takwimu Afrika yatakayofanyika katika Ukumbi wa CHuo cha utalii Maruhubi pamoja na mechi ya mpira wa miguu itakayofanyika wakati wa jioni katika viwanja vya Maudsetung kati ya Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali na timu ya Benki ya watu wa Zanzibar PBZ.
Siku ya Takwimu Afrika itaadhimishwa kwa kauli mbiu isemayo ''uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa eneo huru la biashara la bara la Afrika (AfCFTA); mchango wa takwimu rasmin na Big data katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya Afrika jukumu la takwimu rasmi na Takwimu kubwa katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya Afrika".
Kauli mbiu hiyo inawiana ns kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2023 iliyohimiza "kuharakisha utekelezaji wa AfCFTA",na inajumuisha wito wa kuboresha mifumo ya data katika bara la Afrika ili kuzalisha na kutumia takwimu rasmi za ubora wa hali ya juu na kuchangamkia fursa zitokanazo na 'big data'/ takwimu rasmi.
See Insights
Boost a Post
Like
Comment
Share