Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar
Wananchi wameahidiwa kuwepo kwa maonyesho yakipekee yatakayo jumuisha wafanya biashara nchini na nje ya nchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Bishara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mh Omar Said Shaaban wakati akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake kinazini Wilaya ya Mjini Unguja kwa lengo la kutoa taarifa juu ya maandalizi ya 10 ya kimataifa pamoja na kuzindua rasmi wa nembo mpya ambayo itakayowezesha maonyesho hayo kuendelea mbele.
Amesema lengo kubwa la maonyesho hayo ni kutoa fursa kwa wananchi hususan wafanya biashara ndani na nje ya nchi kuonesha bidhaa wanazouza na wanazotengeneza hapa nchini.
Hata hivyo amesema kuwa maonesho hayo ya kipekee yanatoa fursa kwa taasisi mbali mbali za Serikali kutoa huduma zenye mnasaba wa kibiashara.
Ameendelea kwa kusema kuwa kwa mwaka 2024 Serikali nchini itakua inatimiza miaka 60 ya Mapinduzi Zanziba hivyo Wizara ya biashara hainabudi kufanya maonesho hayo kutokana na ukubwa wa miaka iyo ya mapinduzi.
Pia amesema kuwa tangu kuingia kwa uongozi wa Serikali ya awamu ya nane ya uongozi wa Dkt. Husein Ali Mwinyi Serikali iliahidi kuendeleza mradi wa viwanda vya maonesho katika maeneo ya Nyamamzi Dimani.
Kwa kawaida maonesho hayo yanafanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja lakini kwa mwaka huu 2024 maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Nyanmazi Dimani kwani eneo hilo ni lakudumu na pia kutakua na muendelezo wa maenyesho yasiyopungua matatu ndani ya mwaka.
Maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 7 Januari 2024 na kumalizika tarehe 19 Januari 2024 kwa kawaida yanafanyika kila mwaka na kuambatana na shamra shamra za sherehe za Mapinduzi Zanziba ambapo sasa inatimiza miaka 10 tangu kuasisiwa kwa maonyesho hayo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Biashara mtandao kwa maendeleo ya biashara na utekelezaji.
0 Comments