Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar

Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja wafurahia zaidi uwepo wa bararabara mpya za ndani zilizojengwa hivi katibuni kufuatia Uongozi wa Rais wa awamu ya nane ya Rais wa Zanzibar Mh. Hussen Ali Mwinyi.
Hayo yamejiri baada ya kufanyika ziara ya siku mbili ya waandishi wahabari pamoja na wakala wa ujenzi wa barabara hizo na kufanya mahojiano na wananchi mbali mbali katika mikoa hiyo.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwamvua Ali Makame Mkaazi wa Shaani Kaskazini Unguja amesema wamenufaika sana kwa uwepo wa barabara mpya katika makaazi yao kwani hapo awali kulikua na changamoto nyingi lakini kwa sasa wanauwezo mkubwa wa kufanya harakati zao za kilimo na biashara kwa ufanisi mkubwa.
Nae Hamadi Yussuf Tabu mkaazi wa Matemwe Kilima Juu amesema hapo awali kulikua na changamoto kwa wananchi kutokana na Wembamba wa njia lakini baada ya kupatikana kwa barabara katika kijiji hicho shuhuli za wananchi zinaendelea ipasavyo.
Kwaupande wake mkaazi wa kijiji cha Kajengwa Makunduchi Simai haji Ali amesema hapo awali kulikua na changamoto ya gari za abiria kugoma kufika baadhi ya maeneo kutokana na kutokua na ubora wanjia lakini baada ya kupatikana barabara hizo imekuwa ni faraja kubwa kwani nikilio


chamuda mrefu kimeweza kupatiwa ufumbuzi.
Nae Issa Salum Muhammed mwanaharakati wa uendeshaji wa boda boda amesema hapo awali njia ilkua ninyembamba ilipelekea hata gari za abiria kutofika baadhi ya maeneo hatimae wananchi kutafuta usafiri wa bodaboda lakini kwa sasa njia imekua pana kiasi ambacho inauwezo mkubwa wa kupita vyombo mbali mbali vya moto.
Kaimu Mkurugenzi wakala wa barabara Zanziba Cosmos Masolwa amebainisha kuwa Ujio wa Uongozi wa awamu ya nane wa Rais wa Zanziba na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi wa Dkt. Husein Ali Mwinyi umefanya mabadiliko ya kipekèe ya miundombinu ya barabara kwani wananchi katika kero kubwa waliokua wakilalamika ni kuepo barabara hususan barabara za ndani.

Hata hivyo Kaimu huyo amewataka wananchi kuzitumia vyema barabara hizo pamoja na kuwa na subira ya kusubiria hatua zamwisho za kumalizika kwa barabara hizo.
Miongoni mwa barabara ambazo zilizobahatika kufanyiwa ziara iliyojumuisha waandishi pamoja na wakala wa barabara Zanziba ni pamoja na barabara ya Donge vijibweni hadi chaani Masingini,Matemwe mfurumatonga hadi matemwe Kilima juu,Upenja kibumbini,Mchangani Dogongwe, Bumbisudi Kizimbani pamoja na Makunduchi Kajengwa Kusini Unguja ambao ujenzi huo unasimamiwa na Kampuni ya IRIS kutoka Uturuki.