Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania DK. Philips Isdor Mpango amesema ikiwa Tanzania ipo katika harakati za mabadiliko ya huduma za afya imejipanga katika kuwekeza kupitia sekta ya matibabu.
Nae Waziri wa Afya wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Ummi Ali Mwalim amewasisitiza wananchi kuzingatia pamoja na kufuata ushauri wa madaktari katika kuacha matumizi ya pombe na kuzingatia ulaji wa vyakula ili kuepuka magonjwa ya moyo na Figo ambayo yamekuwa na kiwango kikubwa cha gharama katika matibabu yake.
Amesema ikiwa Serikali inawekeza katika sekta ya matibabu ipo haja ya kuwekeza katika huduma za kinga kwani ni vyema kujuwa kuwa kinga nibora kuliko tiba hivyo amewataka wanamafunzo hao kutofanya mzaha katika mafunzo hayo.
Nae mtendaji wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Dk.Peter Richard Kisenge amesema kuwa ukubwa wa tatizo la ugonjwa huo wa moyo umepelekea Serikali kuanzisha Taasisi ambayo ni mfano kwa Afrika Mashariki katika kutoa huduma zilizo bora.
Mkutano huo wa kisayansi wa masuala ya matibabu ya moyo ambao ulioandaliwa na taasisi ya Jakaya kikwete kwa kushirikiana na wadau mbali mbali umeshirikisha zaidi ya wataalamu mia tano na miongoni mwa mada kuu wanayoijadili ni namna ya kujikinga na maradhi ya moyo.
0 Comments