MAKALA YA CHANJO
CHANJO NI NINI, NA INAFAIDA GANI KWA WATOTO?
Inaelezwa kuwa Chanjo huokoa maisha ya hadi watoto milioni 3 kila
mwaka,Chanjo humlinda mtoto dhidi ya magonjwa hatari, hujenga kinga,
huzuia milipuko, na kupunguza gharama za huduma za afya.
Chanjo hukinga maradhi, ulemavu na vifo vitokanavyo na magonjwa
yanayozuilika kwa chanjo ikiwa ni pamoja na surua, homa ya ini
(hepatitisi B), dondakoo, kifaduro, nimonia, polio, kuhara
kunakosababishwa na virusi vya rota, rubela na pepopunda.
Kisayansi chanjo ni kitendo cha kupewa kinga mwili kwa njia ya kuamsha
vitoa kinga viwe tayari kupambana na adui ambaye wanamjua tayari
UMUHIMU WA CHANJO.
UMUHIMU WA CHANJO.
Chanjo zina umuhimu mkubwa kwani Watoto waliopata chanjo huwa
wamekingwa dhidi ya magonjwa hatari, ambayo kwa kawaida huweza
kusababisha ulemavu au kifo,Watoto wote wana haki ya kupata kinga
hii,kinga ya utotoni ni muhimu sana hasa kwa ukuaji wa baadae.
Hivyo basi, chanjo kwa mtoto katika mwaka wake wa kwanza na katika
mwaka wa pili ni muhimu sana ,ni muhimu pia, kina mama wajawazito
kupata chanjo ya pepopunda ili kujikinga wao wenyewe na watoto wao
wanaozaliwa.
Wazazi na walezi wengine wanapaswa kufahamu sababu za umuhimu wa
chanjo, ratiba ya chanjo inayotumika na mahali chanjo inakotolewa kwa
watoto,Wazazi na walezi wengine wanapaswa kufahamu kuwa kutoa chanjo
kwa mtoto mgonjwa kidogo au mwenye ulemavu au mwenye upungufu wa lishe
ni salama.
UKWELI KWA AJILI YA FAMILIA NA JAMII KUHUSU CHANJO
1.Chanjo ni jambo la lazima, kila mtoto ni lazima apate chanjo zote
zilizopendekezwa,kinga ya utotoni ni muhimu sana;
Chanjo katika mwaka wa kwanza na wa pili zina umuhimu wa pekee,Wazazi
wote au walezi wengine wanapaswa kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa
afya kuhusu muda wa kukamilisha chanjo zinazohitajika.
2. Chanjo hutoa kinga dhidi ya magonjwa mengi hatarishi. Mtoto ambaye
hajapata chanjo yuko katika hatari kubwa ya kupatwa na maradhi,
ulemavu wa kudumu au hata kupoteza maisha.
3. Mama wote wajawazito pamoja na watoto wao wanapaswa kukingwa dhidi
ya pepopunda,hata kama mama aliwahi kupata chanjo kabla , anapaswa
kupata ushauri wa mtaalamu wa afya kuhusu kama bado anahitaji kupewa
chanjo ya pepopunda.
4. Sindano mpya hazina budi kutumika kwa kila mtu anayepata chanjo,
kila mtu anapaswa kudai sindano mpya kwa kila chanjo anayopewa.
5. Ugonjwa huweza kuenea haraka watu wengi wanapokuwa wamekusanyika
pamoja, Watoto wote wanaoishi katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa ,
hasa katika mazingira ya wakimbizi au ya watu waliojikusanya kutokana
na janga fulani, wanapaswa kupewa chanjo haraka.
6. Kadi ya chanjo ya mtoto (au ya mtu mzima) haina budi kuwasilishwa
kwa mtoa chanjo kabla ya kutolewa kwa chanjo.
AINA ZA CHANJO
BCG (BACILE CALMETTE-GUÉRIN)
Watoto wote wanastahili kupokea chanjo itwayo BCG (Bacile
Calmette-Guérin) vaccine, hii huumpa mtoto kinga dhidi ya aina zingine
za kifua kikuu na ukoma.
DTP AU DPT (DONDAKOO, PEPOPUNDA NA KIFADURO)
Watoto wote wanastahili chanjo dhidi ya dondakoo, pepopunda na
kifaduro kupitia aina ya chanjo iitwayo DTP au DPT vaccine, Viini vya
dondakoo husababisha maambukizi ya njia ya kuingizia hewa na huenda
ikasababisha shida za kupumua na hata kifo.
Pepopunda nayo husababisha kukauka kwa misuli na maumivu makali yanayo
sababishwa na mkazo wa misuli. Mkazo huo wa misuli unaweza sababisha
kifo.
Kifaduro huathiri njia ya kuigizia hewa na kusababisha kikohozi
kinachoweza dumu wiki nne hadi nane na ni hatari sana kwa watoto
wachanga.
Wanawake wote waja wazito na watoto wachanga wanahitaji chanjo ya pepopunda.
SURUA.
Watoto wote wanastahili kupokea chanjo dhidi ya surua. Maradhi ya
surua husababisha utapiamlo, udhaifu wa maendeleo ya ubongo na huweza
kufanya mtoto kiziwi au kipofu.
Ishara zinazoelekeza kuwa mtoto anaweza kuwa anaugua surua ni pamoja
na kuongezeka kwa joto mwilini, upele, kikohozi, kumwaga kamasi na
macho kubadilika na kuwa mekundu. Tahadhari, mtoto anaweza kufa
kutokana na surua.
POLIO
Watoto wote wanastahili chanjo dhidi ya polio kwani Dalili za polio ni
utepe kwenye mguu au mkono na udhaifu wa kukitumia kiungo kilicho
athirika, kwa kila watoto mia mbili wanaoambukizwa maradhi ya polio,
mmoja hupata ulemavu wa maisha.
Ratiba za chanjo hutofautiana kulingana na nchi au sehemu ya nchi
tunavoishi, ni muhimu kufuatilia ratiba ya chanjo kwa mujibu wa
mwongozo wa taifa.
Watoto wanastahili kupokea chanjo kwa umri unaostahili na kwa muda
unaostahili,pamoja na kutofautiana huku kwa ratiba za chanjo kati ya
nchi na nchi, unaweza kufuatilia utaratibu uliopendekezwa na CDC
(Centre for Disease Control) hapa chini.
Ufuatao ni mtiririko wa chanjo husika na wakati muafaka ambao mtoto
wako anatakiwa awe ameshapatiwa.
UMRI
AINA YA CHANJO
INATOLEWAJE
MUHIMU KUJUA
0 – Anapozaliwa
Kifua Kikuu (BCG)
Sindano bega la kulia
Ni lazima kovu lotokee kwenye bega la kulia baada ya muda
Polio (OPV 0)
Matone mdomoni
Chanjo ya ugonjwa wa kupooza ya kuanzia
Wiki ya 6
Polio (OPV 1)
Matone mdomoni
Chanjo ya kwanza ya ugonjwa wa kupooza
DTB-HepB-Hib1 (Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda na Hepatiti B)
Sindano paja la kushoto
Chanjo ya kwanza ya Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda na Hepatiti B kwa pamoja.
PCV 1
Sindano paja la kulia
Chanjo ya Nimonia ya kwanza
Rota 1
Matone mdomoni
Chanjo ya Kuhara ya kwanza
Wiki ya 10
Polio (OPV 2)
Matone mdomoni
Chanjo ya pili ya ugonjwa wa kupooza
DTB-HepB-Hib2 (Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda na Hepatiti B)
Sindano paja la kushoto
Chanjo ya pili ya Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda na Hepatiti B kwa pamoja.
PCV 2
Sindano paja la kulia
Chanjo ya Nimonia ya pili
Rota 2
Matone mdomoni
Chanjo ya kuhara ya pili
Wiki ya 14
Polio (OPV 3)
Matone mdomoni
Chanjo ya mwisho ya ugonjwa wa kupooza
DTB-HepB-Hib3 (Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda na Hepatiti B)
Sindano paja la kushoto
Chanjo ya tatu ya Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda na Hepatiti B kwa pamoja.
PCV 3
Sindano paja la kulia
Chanjo ya Nimonia ya tatu
Miezi 9
Measles (MR 1)
Sindano bega la kushoto
Chanjo ya kwanza ya surua
Miezi 15
Measles (MR 2)
Sindano bega la kushoto
Chanjo ya pili ya surua
Kwa upande wake Ofisa Chanjo Wilaya ya Chake Chake Pemba Fihim
Abdalla Moh’d anasema mwamko wa wazazi katika kuwapeleka watoto kupata
Chanjo kwa wilaya hiyo ni wastani kwani kila mwezi hutakiwa kuchanja
watoto kwa asilimia 95% lakini badala yake wanachanja kwa asilimia 78%
tu.
Anaeleza ili waweze kufikia lengo lililowekwa kuna mambo mbali mbali
ambayo yanatakiwa kufanywa ili liweze kufikiwa lengo la kuchanja
watoto kwa asilimia 95% na kuwafanya watoto waweze kuwa na afya
inayotokana na kupata Chanjo.
Anayataja mambo hayo kuwa ni wazazi kufuata ratiba ya chanjo kwa
kuanza na kukamilisha chanjo wenyewe kwani hayo ni mambo mawili
tafauti ambayo yote yana madhara.
Anasema kuwa jambo jengine ni kwa madaktari wenyewe kuwa makini
katika kutowa Elimu kwa wazazi wanaohudhuria Klinik kwa ajili ya
Chanjo, pia Masheha na wahudumu wa Afya za Jamii CHV kuandaa mikutano
na kuielisha jamii umuhimu wa Chanjo kwa watoto.
‘’ Kila mwaka kama kitengo cha Chanjo tunafanya vikao vitatu na
viongozi wa Dini mbali mbali ili kuelimisha umuhimu wa chanjo kupitia
waumini wao hasa katika hotuba zao’’, anasema.
Anasema mpaka sasa ndani ya Wilaya ya Chake Chake hakujatokea madhara
ya moja kwa moja kwa mtoto ambae hakupata chanjo ama hakukamilisha ,
ispokuwa kunatokea dalili za Surua na hii wanapofuatilia hugundua ni
kwa wale watoto ambao hawakupata chanjo ama hawakukamilisha .
Ofisa huyo anatowa wito kwa jamii kwanza kuwa na utayari kwa wazazi
kuwapeleka watoto wao kupata chanjo na uthubutu wa wazazi
kuwakamilishia.
Aidha anawataka Wazazi kuwa na tabia ya kuhamasishana kuwapeleka
watoto wao kupata chanjo na umuhimu wake kwa watoto katika kulinda
afya zao wakiwa wadogo hata ukubwani.
‘’ Kuna tatizo kwa baadhi ya akinababa hasa wa Vijijini kuwazuwia
wazazi wenzao wa kike kuwapaeleka watoto kwa ajili ya kupatiwa chanjo,
jambo ambalo linapunguza malengo ya Serikali katika kuwapatia watoto
huduma ya Chanjo’’, anasema.
Mama Halima Said Moh’d mkaazi wa Wingwi anasema akinamama wenye mwamko
wa kuwapaleka watoto wao Kilinik kwa kupata huduma ya Chanjo wamekuwa
wakipungukiwa na maradhi ya mara kwa mara kwa watoto wao hasa wale
ambao wanakamilisha Chanjo kwa maujibu wa taratibu za Wizara ya Afya.
Anaeleza kuna sababu mbalimbali za kumchanja mtoto katika umri
tafauti ,kwa vile kuna faida za chanjo ya mtoto kwa kumkinga na
maradhi mbali mbali ikiwemo ya kuambukiza, kwani zina umuhimu kwa
ulinzi wa afya yake kwa ujumla.
Hata hivyo Chanjo ya mtoto inahusisha kutoa chanjo ili kumlinda mtoto
dhidi ya aina mbalimbali ya magonjwa ya kuambukiza na hufanya kazi
kwa kuchochea mfumo wa kinga kutambua na kupigana na vimelea maalum
MWISHO.
Imetayarishwa na Bakar Mussa
Na kwa msaada wa Mtandao
bekamussa3@gmail.com.

0 Comments