WANAWAKE WAPATA UJASIRI KUYAKABILI MABADILIKO YA TABIANCHI

Wakulima viongozi waliopatiwa mafunzo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuwawezesha wanawake katika uongozi kupitia mradi wa Zan adapt kwenye kilimo msitu na upandaji wa mikoko Pemba T.O.T wamesema wamepata njia ya kujenga uwezo na ujasiri kujitegemea na uongozi imara.
Wametoa kauli hio walipokua wakizungumza na Waandishi wa habari hizi huko Gombeume mchangamdogo na kuelezea halihalisi ya mradi huo na changamoto zinazowakabili.

Akizungumza Zaituni Hassan Ali ambae ni mkulima wa bonde la Gombeume mchangamdogo amesema ili kuweza kuionesha  njia ya mafanikio kwa wanawake ni kujitumia vyombo vya habari katika na sambamba na wao kujiingiza katika kilimo msitu kwa vitendo ni moja ya mafanikio kwao ambayo wameyafikia.
Amesema imani yake endapo wataendelea kuvitumia vyombo hivyo wataweza kusikika kwa haraka na kutatuliwa changamoto zao zinazowakabili katika kilimo hicho.

Amesema kuwa kilimo msitu ni mkombozi za wanawake kwani kitaweza kuwabadilisha maisha yao kutoka hali duni na kuwapelekea kuwa na kipato.

Fatma Hamad Bakar mkulima wa bonde hilo pia amesema mradi wa Zan adapt umechukua hatua madhubuti katika kuwainua wanawake kwa kukuwapatia zana, ujuzi rasilimali na nafasi za uongozi katika kilimo endelevu na mazingira.
Amesema kupitia mradi huo sasa wanawake wamekua mabalozi wa mazingira ya kiuchumi katika jamii zao kwani wamejiitika katika kilimo na kuingia katika kuomba nafasi za uongozi bila ya hofu.

Akitaja miongoni mwa changamoto zinazowakabili katika mradi huo Fatma Saidi Haji amesema pamoja na mabadiliko ya tabianchi yasiotabirika ikiwemo mvua  zisizokua na msimu na jua kali ambapo huathiri kilimo hicho.

Amesema ukosefu wa Miundombinu ya maji na Umwagiliaji wa kudumu  kunawapelekea kubeba maji kutoka kwenye visima jambo ambalo ni gumu na kurejesha nyuma uzalishaji wa kilimo.

Akitaja baadhi ya mikakati wanayoifanya ni kutoa elimu juu ya kujikita na kilimo hicho, kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi hata katika ngazi za nchi na kuacha mitazamo finyu inayodhoofisha ushiriki wa wanawake katika maamuzi ya kijamii na miradi ya kimaendeleo .

Ali Bakari amesema pamoja na mradi huo kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanawake kuendeleza kilimo hicho changamoto zinahitaji kushughulikiwa kwa haraka ili kuhakikisha mafanikio ya mradi yanatakelezeka na kuwanufaisha vizazi vijavyo.
Mradi huo wa Zan adapt unaolenga kuwanyanyua wanawake kiuongozi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye kilimo msitu ambao unatekelezwa kwa maeneo manne kisiwani Pemba

Post a Comment

0 Comments